Main Page

Download
About Islam
Islamic Pillars
Prophetic Tradition
Islamic Encyclopedia
Non-Muslims
Legislation
Creed
Prophet's Stories
Islamic history
Islamic Architecture
Library
Islamic conferences
Islamic conferences
   Qurani /6- SURAT AL AN AAM/
 
Aya 19

19- Ewe Nabii! Waambie wale wanaokukadhibisha na wanaotaka ushahidi wa ujumbe wako: Kitu gani ushahidi wake ndiyo mkubwa kabisa na chenye kustahiki kusadikiwa kuliko vyote? Kisha sema: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Shahidi Mkubwa kushinda wote wa kushuhudia baina yangu na baina yenu kuhusu ukweli wa haya niliyokuleteeni. Na Yeye ndiye Aliyeniteremshia Qurani hii ili iwe ni hoja ya ukweli wangu, nipate kukuhadharisheni nyinyi na kila itakayomfikia habari yake. Nayo ni hoja ya kweli inayoshuhudia ukweli wangu kwani nyinyi hamwezi kuleta mfano wake. Waulize: Je, hivyo nyinyi ndio mnasema kwa yakini kwamba Mwenyezi Mungu Ana miungu wengine pamoja naye? Kisha waambie: Mimi sishuhudii hayo wala sisemi hivyo wala sikukubalieni kwa hayo. Hapana shaka wa kuabudiwa kwa haki ni Mungu Mmoja tu. Na mimi niko mbali na hayo masanamu mnayomshirikisha naye.

Previous         Next

Main Page Contact us Links About us Site Map