Qurani
/
6- SURAT AL AN AAM/
Aya 39
38-39- Na bila shaka dalili ya nguvu zaidi juu ya Uwezo wa Mwenyezi Mungu, hekima Yake na rehema Zake, ni kwamba Yeye Amekiumba kila kitu. Na hakuna katika ardhi mnyama anayetambaa juu ya uso wake au ndani yake, au ndege anayeruka hewani kwa mbawa zake, isipokuwa wote hao Mwenyezi Mungu Amewaumba makundi makundi yanayofanana nanyi na akayapa sifa maalumu, sifa za kipekee na mfumo maalumu wa maisha. Hatujakiacha chochote katika Kitabu kilichohifadhiwa Kwetu isipokuwa Tumekithibitisha. Na ingawa wao wamekadhibisha, lakini hata hivyo, watakusanywa na makundi yote kwa ajili ya hisabu siku ya kiyama. Na wale ambao hawajaziamini hoja Zetu zenye kuonyesha uwezo Wetu na ukweli wa risala yako, hawatanufaika kwa viungo vyao vya hisia katika kuijua haki. Matokeo yake itakuwa ni kubabaika katika upotevu wa ushirikina na ukaidi kama anavyojigongagonga mtu kiziwi bubu katika giza la usiku. Mtu huyu ni lazima aangamie. Na lau kama watu hawa wangalikuwa tayari kwa ajili ya kheri, basi Mwenyezi Mungu Angaliwafanikishia. Kwani Yeye Subhana Anapotaka kumpoteza mtu aliyeuharibu mwelekeo wake, basi Humwacha hivyo hivyo alivyo. Na Anapotaka kumwongoa mwenye mwelekeo sahihi, Humrahisishia mwendo katika njia ya imani iliyowazi na iliyonyooka.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map