Main Page

Download
About Islam
Islamic Pillars
Prophetic Tradition
Islamic Encyclopedia
Non-Muslims
Legislation
Creed
Prophet's Stories
Islamic history
Islamic Architecture
Library
Islamic conferences
Islamic conferences
   Qurani /6- SURAT AL AN AAM/
 
Introduction

(Imeteremka Makka na aya zake 165)

Ni sura iliyoteremka Makka isipokuwa aya hizi: 20, 23, 91, 93, 114, 
141, 151, 152 na 153. Ilishuka baada ya Surat Al Hijri na jumla ya 
aya zake ni 165.
Sura hii takatifu imekusanya maana mbalimbali ilizozichambua.
- Imewazindua watu juu ya ulimwengu na vielelezo vilivyomo ndani 
yake vinavyoashiria utukufu wa Muumbaji wake na upweke Wake 
na kwamba hashirikiani naye yeyote katika uumbaji wala 
kuabudiwa  wala dhati.
- Ina visa vya baadhi ya Manabii. Sura imeanza kwa kisa cha 
Ibrahimu (A.S) ikibainisha kwamba yeye alichukua maana ya ibada 
na Upweke wa Mwenyezi Mungu kutokana na kuutafakari kwake 
ulimwengu na kuyachungua kwa kina yaliyomo ndani yake. Alianza 
kuzichungua nyota, halafu mwezi, kisha jua na hatimaye akaishilia 
kumwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.
- Imeyaelekeza macho kuyaangalia maajabu ya uumbaji na 
utengenezaji. Imebainisha ni vipi kihai kinyevu kinamea toka 
kwenye kiumbe kikavu kisicho na uhai, na ni vipi punje 
inavyopasuka na kuwa ni mmea.
- Imezitaja sifa za makaidi na ni vipi wanavyong’ang’ana na dhana 
zinazowapoteza na kuwaweka mbali na haki.
- Kuna ufafanuzi juu ya halali Aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu 
katika vyakula na upotevu wa washirikina katika yale 
waliyojiharamishia wenyewe bila ya kuwa na dalili, na ni vipi 
wanavyomnasibishia Mwenyezi Mungu uharamishaji.
- Kuna ufafanuzi juu ya maamrisho haya yafuatayo ambayo ndiyo 
Uislamu wenyewe hasa na mienendo mema:
Kuharamisha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kufanya zina, kuua 
na kula mali ya yatima. Pia wajibu wa kupima kamili bila kupunja 
katika vipimo na mizani, kuhakiki uadilifu, kutekeleza ahadi, 
kuwatendea wema wazazi wawili na kuzuia kuwazika hai watoto 
wachanga wa kike.

        Next


(Imeteremka Makka na aya zake 165) Ni sura iliyoteremka Makka isipokuwa aya hizi: 20, 23, 91, 93, 114, 141, 151, 152 na 153. Ilishuka baada ya Surat Al Hijri na jumla ya aya zake ni 165. Sura hii takatifu imekusanya maana mbalimbali ilizozichambua. - Imewazindua watu juu ya ulimwengu na vielelezo vilivyomo ndani yake vinavyoashiria utukufu wa Muumbaji wake na upweke Wake na kwamba hashirikiani naye yeyote katika uumbaji wala kuabudiwa wala dhati. - Ina visa vya baadhi ya Manabii. Sura imeanza kwa kisa cha Ibrahimu (A.S) ikibainisha kwamba yeye alichukua maana ya ibada na Upweke wa Mwenyezi Mungu kutokana na kuutafakari kwake ulimwengu na kuyachungua kwa kina yaliyomo ndani yake. Alianza kuzichungua nyota, halafu mwezi, kisha jua na hatimaye akaishilia kumwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake. - Imeyaelekeza macho kuyaangalia maajabu ya uumbaji na utengenezaji. Imebainisha ni vipi kihai kinyevu kinamea toka kwenye kiumbe kikavu kisicho na uhai, na ni vipi punje inavyopasuka na kuwa ni mmea. - Imezitaja sifa za makaidi na ni vipi wanavyong’ang’ana na dhana zinazowapoteza na kuwaweka mbali na haki. - Kuna ufafanuzi juu ya halali Aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu katika vyakula na upotevu wa washirikina katika yale waliyojiharamishia wenyewe bila ya kuwa na dalili, na ni vipi wanavyomnasibishia Mwenyezi Mungu uharamishaji. - Kuna ufafanuzi juu ya maamrisho haya yafuatayo ambayo ndiyo Uislamu wenyewe hasa na mienendo mema: Kuharamisha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kufanya zina, kuua na kula mali ya yatima. Pia wajibu wa kupima kamili bila kupunja katika vipimo na mizani, kuhakiki uadilifu, kutekeleza ahadi, kuwatendea wema wazazi wawili na kuzuia kuwazika hai watoto wachanga wa kike.

 
Main Page Contact us Links About us Site Map