Qurani
/
8 - SURAT AL ANFAL/
Aya 1
1- Nabii alitolewa Makka akihama kutokana na vitimbi na njama walizozipanga washirikina ili kumwua na ili Waislamu wawe na dola yao. Nabii alifikia Madina kukaa kwenye amani na kupata usaidizi.Ilikuwa ni lazima kupigana jihadi kwa ajili ya kuuzuia uadui na ili Waislamu wasiingie katika mtihani mgumu. Na hapo ndipo vikawa vita vikuu vya Badri. Ushindi mkubwa ukapatikana pamoja na ngawira nyingi. Ngawira hizi zikaleta mivutano ya hapa na pale na maswali juu ya namna ya kuzigawanya. Wanakuuliza juu ya ngawira. Ni wapi zitakwenda? Zitakuwa ni za nani? Na ni vipi zitagawanywa?Basi waambie ewe Nabii! Kwanza kabisa ngawira hizi ni za Mwenyezi Mungu na Mtume. Na Mtume ndiye atakayesimamia suala la ugawaji wake kwa amri ya Mola wake. Kwa hivyo, acheni kuzozana juu ya ngawira hizo. Kufanyeni kumwogopa Mwenyezi Mungu na kumtii kuwe ndiyo nembo yenu, na suluhishaneni kati yenu. Yafanyeni mahusiano kati yenu kuwa ni mapenzi na uadilifu, kwani hii ndiyo sifa ya Waumini.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map