Qurani
/
8 - SURAT AL ANFAL/
Introduction
(Imeteremka Madina na aya zake 57) Sura hii iliteremka Madina. Ina aya 75. Katika sura hii, Mwenyezi Mungu Amezibainisha baadhi ya hukumu za vita, sababu zake, njia za kupatia ushindi, ngazi ya nguvu ya kimorali katika kushinda vita, hukumu za ngawira za vita na wakati wa kuwa na mateka. Sura hii pia vile vile, inaelezea kisa cha vita vya Badri na baadhi ya matukio yaliyokuwa kabla yake na yale yaliyofuatia katika kuashiria sababu yake. Nayo ni kuondoshwa Mtume Makka na washirikina. Aidha, Mwenyezi Mungu Anataja ndani yake kujiandaa kwa vita na wajibu wa kushikamana na amani kama maadui wataielekea. Sura Takatifu, inamalizia kwa kubainisha kusaidiana na kuchungiana maslaha Waislamu wenyewe kwa wenyewe na ulazima wa kuihama Waislamu sehemu ambayo wananyanyaswa ili wapate nafasi ya kupigana jihadi na wenzao Waumini katika njia ya kukiweka juu cheo cha Uislamu na cheo chao.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map