Qurani
/
7- SURAT AL - ARAAF /
Introduction
(Imeteremka Makka na aya zake 206) Sura hii imeteremka Makka ila aya nane. Aya hizo ni kutoka aya ya 163 hadi ya 170. Na jumla ya aya za sura ni 206. Mwanzo wa sura hii unaunganisha yale yaliyokuja mwishoni mwa Surat Al An’aam. Kisha ikaanza kuelezea mwanzo wa kuumbwa binadamu. Ikataja kisa cha kuumbwa kwa Adamu na Hawa, na vipi walivyotoka kwenye pepo kwa sababu ya kutiwa wasiwasi na shetani, na ikaeleza wasiwasi huo unaoendelea kwa watu katika mavazi na vyakula. Kisha, kama zilivyo sura nyingine za Qurani, aya za sura hii tukufu zimegusia kutazama mbingu na ardhi kwa kuyazingatia yaliyomo ndani yake kati ya utaratibu wa ajabu. Vilevile, sura hii imeviashiria visa vya Manabii kama Nuh na Hud pamoja na kaumu yake ’Aad. Kisha kisa cha Saleh pamoja na kaumu yake Thamud waliosifika kwa nguvu na kupewa utajiri. Pia kisa cha Lut na kaumu yake na vipi walivyokuwa wakifanya maovu. Na mwisho kisa cha Shu’aib pamoja na watu wa Madyana. Kisha sura hii imeeleza visa vya kweli na mafunzo na pamoja na mazingatio yaliyomo ndani yake. Na baada ya hayo, Mwenyezi Mungu Subhana Ametaja kisa cha Musa na yaliyotokea katika mambo ya Firauni. Na sura imemalizikia kwa kutoa taswira ya hali ya mwenye kupewa uongofu halafu akabanduka akaingia kwenye upotovu kwa kumfuata shetani na njia zake. Kisha sura imeelezea mwito wa haki aliokuja nao Muhammad (S.A.W).
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map