Qurani
/
2- Surat AL - BAQARAH /
Aya 3
3- Na hawa, ndio wale wanaoyaamini mambo ya ghaibu kwa kunyenyekea, na wanayaamini mambo yaliyo nje ya upeo wa viungo vya hisi kama malaika na siku ya mwisho kwani msingi wa kushika dini ni kuamini ghaibu. Pia, wanatekeleza sala sawa sawa kwa kumwelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu kamili na wanatoa sehemu katika vile Alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu katika milango ya kheri na wema.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map