Qurani
/
11-SURAT HUD/
Aya 29
29- Enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali kwa ajili ya kuufikisha ujumbe wa Mola wangu, bali naomba malipo yangu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala mimi siwafukuzi kwenye baraza yangu na kutangamana nami waliomwamini Mola wao kwa sababu ya kuwa nyinyi mnawadharau tu! Kwani wao watakuja kukutana na Mola wao siku ya kiyama, basi watanishitaki Kwake ikiwa nimewafukuza kwa ajili ya ufakiri wao. Lakini mimi nakuoneni nyinyi ni watu msiojua jambo linalofaa viumbe kuzidiana ubora Mbele ya Mwenyezi Mungu! Je, ni utajiri na cheo kama mnavyodai? Au kuifuata haki na kufanya kheri?
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map