Qurani
/
11-SURAT HUD/
Aya 3
3- Mnyenyekeeni Mwenyezi Mungu na huku mnamwomba Akusameheni madhambi yenu. Kisha rejeeni Kwake kwa kumwabudu kwa ikhlasi na kufanya vitendo vyema ili Apate kukustarehesheni starehe nzuri duniani mpaka utakapomalizika muda wenu uliokadiriwa, na apewe huko akhera kila mwenye vitendo vyema vilivyo bora malipo ya kazi yake na fadhila yake. Na ikiwa mtayaacha haya ninayokuitieni kwayo, basi mtajiletea adhabu. Na mimi nakuhofieni adhabu hii katika siku kubwa watakapokusanywa watu wote na kutokea kitisho kikubwa kabisa.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map