Qurani
/
11-SURAT HUD/
Aya 9
9- Na katika tabia ya binadamu, ni kujizamisha mwenyewe katika hali aliyonayo. Basi Tukimpa baadhi ya neema kwa huruma Yetu kama vile afya nzuri na ukunjufu wa riziki, kisha baadaye Tukamwondolea neema hizo kwa mujibu wa mipango Yetu, yeye hupita mipaka katika kukata tamaa kuwa neema hiyo haitorudi tena, na akapita mipaka katika kuzikufuru neema nyingine ambazo bado angali anastarehe nazo!
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map