Qurani
/
3- SURAT AL - IMRAN/
Aya 19
19- Bila shaka dini ya haki iliyoridhiwa na Mwenyezi Mungu, ni dini ya Tawhidi (Mungu mmoja tu) na kumnyenyekea kwa usafi wa moyo. Mayahudi na Wakristo wametofautiana na dini hii, wakapotoa na wakabadili. Na haikuwa kutofautiana kwao ni kwa sababu ya kuchanganyikiwa au kwa ujinga, kwa vile elimu imekwishawajia, bali yalikuwa hayo ni kwa sababu ya uhasidi na ukaidi uliokuwa baina yao. Na yeyote anayezipinga Dalili za Mwenyezi Mungu, basi naangojee hesabu ya haraka ya Mwenyezi Mungu.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map