Qurani
/
3- SURAT AL - IMRAN/
Aya 4
4- Aliviteremsha Vitabu hivyo viwili Taurati na Injili kwa ajili ya kuwaongoa watu. Na wakati watu hao walipokengeuka, Aliiteremsha Qurani ili kupambanua kati ya haki na batili na ili kuweka wazi kati ya uongofu na upotevu. Hicho ndicho Kitabu cha ukweli wa daima, na kila anayeyaacha Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ndani yake na kuzikufuru aya Zake, basi ataipata adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mweza kwani Halimshindi jambo na ndiye Mwenye kumlipizia kisasi anayestahiki.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map