Qurani
/
17- SURAT AL-ISRAAI/
Aya 1
1- Mwenyezi Mungu ndiye Aliyetakasika na kila lisilolaiki naye. Yeye ndiye Aliyemchukua mja Wake Muhammad katika sehemu ya wakati wa usiku kutoka msikiti mtakatifu wa Makka kwenda msikiti wa mbali wa Baytul Maqdis ambao Tuliwabarikia wakazi majirani wa msikiti huo katika mahitaji yao ili Tumwonyeshe baadhi ya ishara Zetu zenye ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha upweke Wangu na ukubwa wa uwezo Wangu. Hakika Mwenyezi Mungu Peke Yake ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map