Qurani
/
5- SURAT AL - MAAIDAH /
Aya 2
2- Enyi Waumini! Msiivunje heshima ya utakatifu wa alama za Dini ya Mwenyezi Mungu kama ibada za hija wakati wa ihramu yaani kabla ya kutimiza hija, na vilevile hukumu nyinginezo za sheria. Na wala msivunje heshima ya utukufu wa miezi mitakatifu kwa kuzua moto wa vita katika miezi hiyo. Wala msiwapinge wanyama wanaopelekwa Nyumba Takatifu kuchinjwa kwa kuwapora au kuzuia wasifike huko. Wala msiwaondoe vigwe vilivyofungwa shingoni mwa wanyama hao kwani ni alama kuwa wamekusudiwa kupelekwa Nyumba Takatifu na kuwa watachinjwa wakati wa hija. Wala msiwazuie wanaokusudia kwenda Nyumba Takatifu wakizitafuta Fadhila na Radhi za Mwenyezi Mungu. Na mkishavua mavazi ya ihramu na mkatoka kwenye eneo la Al-haram, basi mnaweza kuwinda mtakavyo. Wala msipelekewe na chuki yenu kubwa kwa wale waliokuzuilieni kufika Msikiti Mtakatifu mkawafanyia uadui. Enyi Waumini! Saidianeni katika kufanya wema na mambo yote ya utiifu na wala msisaidiane katika kutenda maasi na mkapindukia mipaka Aliyoiweka Mwenyezi Mungu. Na iogopeni Adhabu ya Mwenyezi Mungu na nguvu Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuwaadhibu wale wanaoivunja amri Yake.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map