Qurani
/
5- SURAT AL - MAAIDAH /
Aya 3
3- Enyi Waumini! Mwenyezi Mungu Amekuharamishieni kula nyamafu aliyekufa bila ya kuchinjwa kisheria, damu inayotiririka, nyama ya nguruwe na yule ambaye wakati wa kuchinjwa ametajiwa jina lisilo la Mwenyezi Mungu. Pia Amewaharamishieni mnyama aliyekufa kwa kunyongwa, au aliyepigwa mpaka akafa, au aliyekufa kwa kuanguka, au aliyepigwa pembe na mwingine na aliyekufa kwa kujeruhiwa na mnyama mwingine mkali. Ama yule mnyama wa halali kuliwa mnayewahi kumchinja kabla hajakata roho, basi huyo ni halali kwenu. Na Mwenyezi Mungu Amekuharamishieni kula wanyama waliotolewa sadaka kwa ajili ya masanamu. Na Mwenyezi Mungu Amekuharamishieni kutaka kujua yaliyofichikana kwa kuagua kwa mabao (kupiga ramli). Na kula au kutenda chochote kati ya vilivyotajwa kuwa ni haramu, ni dhambi kubwa na ni kutoka kwenye Utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na tangu sasa hivi, makafiri wamekwisha kata tamaa ya kuiondosha dini yenu. Basi msiwaogope kuwa watakushindeni, bali ogopeni kutofuata amri Zangu. Leo Nimekukamilishieni hukumu za dini yenu na kukutimizieni neema Yangu kwa kukupeni nguvu na kukuimarisheni, na Nimekuchagulieni Uislamu uwe dini yenu. Na mwenye kulazimishwa na njaa akala kidogo kati ya vitu hivyo vilivyoharamishwa kwa ajili ya kujiokoa bila ya kukusudia kuasi, basi Mwenyezi Mungu Humsamehe kwa kulazimika kula cha haramu asije akafa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa rehema kwa Alivyovihalalisha.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map