Qurani
/
4- SURAT AN NISAA/
Aya 1
1- Enyi watu! Mcheni Mola wenu Aliyekuumbeni toka kwenye nafsi moja na Akamuumba mkewe kutokana na nafsi hiyo, na kutokana na hao wawili, Akaeneza wanaume na wanawake wengi duniani. Basi nyinyi nyote mnatokana na nafsi hiyo moja! Na mcheni Mwenyezi Mungu mnayemwomba msaada katika kila mnachokihitajia na ambaye pia vile vile mnaombana kwa jina Lake katika mambo yenu. Na waangalieni ndugu wa nasaba wala msiwasusie, sawasawa wakiwa wa karibu au wa mbali, kwani Mwenyezi Mungu daima Hukuangalieni. Hakuna chochote katika mambo yenu kinachofichikana Kwake, kwa hiyo Atakulipeni mlichokifanya.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map