Qurani
/
4- SURAT AN NISAA/
Aya 19
19- Enyi mlioamini! Haifai kwenu kuwafanya wanawake kama bidhaa mkawarithi kwa nguvu bila radhi yao kama ni wake zenu bila ya kuwalipa mahari. Na wala msiwadhulumu kwa kuwabana ili wasamehe sehemu ya mahari mliyowapa. Na wala msiwadhiki ili muwachukulie baadhi ya mali mlizowapa isipokuwa tu kama wakifanya uovu ulio wazi kwa kufanya uasi au kuwa na mwenendo mbaya au kufanya machafu. Ikiwa watafanya hayo, basi ni haki yenu kuwabana au kuchukua baadhi ya mlivyowapa wakati wa kuachana. Na ni juu yenu enyi Waumini, kukaa vizuri na wake zenu kwa maneno na vitendo. Na ikiwa mtawachukia kwa aibu ya kimaumbile au kimwenendo au kwa mengineyo, basi subirini na wala msifanye haraka ya kuwaacha, kwani huenda Mwenyezi Mungu Akatia kheri nyingi ndani ya kile mnachokichukia. Elimu ya mambo yote, ipo kwa Mwenyezi Mungu.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map