Qurani
/
4- SURAT AN NISAA/
Aya 3
3- Na kama mtahofia kuwadhulumu mayatima kwa kuwa ni dhambi kubwa, basi vile vile uogopeni uchungu wa wake zenu kwa sababu ya kutowafanyia uadilifu kati yao mnapooa zaidi ya wanne. Basi oeni wawili, au watatu, au wanne, ikiwa mna imani kuwa mtaweza kufanya uadilifu. Na ikiwa mtaogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja tu, au jistarehesheni na vijakazi mliowamiliki. Kwani hayo ni afadhali kuliko kufanya dhuluma na ujeuri. Na ni afadhali msije mkawa na watoto wengi hatimaye mkashindwa kuwahudumia.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map