Main Page

Download
About Islam
Islamic Pillars
Prophetic Tradition
Islamic Encyclopedia
Non-Muslims
Legislation
Creed
Prophet's Stories
Islamic history
Islamic Architecture
Library
Islamic conferences
Islamic conferences
   Qurani /4- SURAT AN NISAA/
 
Introduction

(Imeteremka Madina na aya zake 176)

Sura hii inazungumzia kwa namna maalumu masuala ya familia na jamii, 
mahusiano kati ya watu, na inaweka hukumu za kuyapangilia mahusiano 
hayo. Imeanzia na familia, kwa vile familia ndio seli ya kwanza ya jamii; 
ikitengenea basi jamii yote itatengenea. Kisha sura baada ya hapo, 
inaingia kuizungumzia jamii na mfumo wake uliokamilika. Na tokea 
mwanzo, sura katika aya yake ya kwanza, inaweka mpaka wa msingi 
ambao mahusiano kati ya watu yanasimamia juu yake. Msingi huo ni 
usawa kati yao. Kwani hakika Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewaumba 
kutokana na nafsi moja, na Akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Kwa 
hiyo, wanadamu wote ni wana wa baba mmoja ambaye ni Adam, na 
mama mmoja ambaye ni Hawa. Wanadamu hawa wanaunganishwa na 
uhusiano wa udugu na usawa. Kwa ajili hiyo, Uislamu unabainisha 
kwamba wanadamu na mpangilio wao, ni kifungu kimoja kinachoanzia 
kwenye familia, kisha kinatanuka na kujumuisha makabila na mataifa 
ambayo inayapasa yajuane na yashikamane kwa namna bora kabisa ya 
kujuana na kushikamana.

        Next


(Imeteremka Madina na aya zake 176) Sura hii inazungumzia kwa namna maalumu masuala ya familia na jamii, mahusiano kati ya watu, na inaweka hukumu za kuyapangilia mahusiano hayo. Imeanzia na familia, kwa vile familia ndio seli ya kwanza ya jamii; ikitengenea basi jamii yote itatengenea. Kisha sura baada ya hapo, inaingia kuizungumzia jamii na mfumo wake uliokamilika. Na tokea mwanzo, sura katika aya yake ya kwanza, inaweka mpaka wa msingi ambao mahusiano kati ya watu yanasimamia juu yake. Msingi huo ni usawa kati yao. Kwani hakika Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewaumba kutokana na nafsi moja, na Akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Kwa hiyo, wanadamu wote ni wana wa baba mmoja ambaye ni Adam, na mama mmoja ambaye ni Hawa. Wanadamu hawa wanaunganishwa na uhusiano wa udugu na usawa. Kwa ajili hiyo, Uislamu unabainisha kwamba wanadamu na mpangilio wao, ni kifungu kimoja kinachoanzia kwenye familia, kisha kinatanuka na kujumuisha makabila na mataifa ambayo inayapasa yajuane na yashikamane kwa namna bora kabisa ya kujuana na kushikamana.

 
Main Page Contact us Links About us Site Map