Qurani
/
13- SURAT AR RAAD/
Aya 2
2- Hakika Aliyekiteremsha Kitabu hichi, ni Mwenyezi Mungu Aliyezinyanyua mbingu mnazoziona zenye nyota zipitazo bila ya nguzo zinazoonwa, wala hazijui mtu ila Mwenyezi Mungu, ijapokuwa Amezifunganisha na ardhi kwa funganisho lisilokatika ila Atakapopenda Mwenyezi Mungu. Na Amelidhalilisha jua na mwezi kwa uwezo Wake kwa ajili ya manufaa yenu. Na jua na mwezi vinazunguka kwa mpango maalumu kwa muda Alioukadiria Mwenyezi Mungu (S.W). Na Yeye Subhana, Anakipanga kila kitu katika mbingu na ardhi na Anakubainishieni ishara Zake za kilimwengu kwa kutaraji mpate kuamini kuwa Yeye ni Mmoja wa Pekee.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map