Qurani
/
13- SURAT AR RAAD/
Aya 3
3- Na Yeye Subhana, ndiye Aliyekukunjulieni ardhi na Akaidhalilisha ili muweze kutembea juu yake mashariki na magharibi. Na Akaweka katika ardhi milima hii iliyosimama imara na mito ya maji matamu inayomiminika. Na Akafanyiza kwa maji hayo matunda ya kabila mbalimbali yanayozaliana, na kati ya kabila hizo kuna namna mbalimbali, mengine matamu na mengineyo machachu, mengine meupe na mengine meusi. Na hakika Yeye Subhana, Huufunika mchana kwa usiku. Na hakika katika ulimwengu huu na maajabu yake, zimo alama za wazi za kuuthibitisha Uwezo wa Mwenyezi Mungu na umoja Wake kwa anayefikiri na akazingatia.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map