Qurani
/
13- SURAT AR RAAD/
Introduction
(Imeteremka Madina na aya zake 43) Surat “Ar Raad” ni sura ya Madina. Imeitwa “Ar Raad” kwa kuzungumzia kwake kwamba radi inamtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na idadi ya aya zake ni 43. Imeanza kwa kukibainisha cheo cha Qurani Tukufu na kwamba imeteremshwa kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha ikaubainisha Ufalme wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika ulimwengu na ikazindua kueleza mambo yaliyoumbwa kwa uzuri na yenye manufaa ndani yake. Kisha ikatoka kuubainisha uwezo Wake Mwenyezi Mungu wa kuumba, ikaingia kubainisha uwezo Wake wa kurejesha tena na kufufua, na Ujuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wa kila kitu, na kuubainisha uwezo Wake wa kuadhibu duniani na kwa hivyo, yaweza kukadiriwa kwa adhabu ya akhera. Kisha sura hii ikaielekeza miono kuyazingatia maajabu ya ulimwengu ya kushangaza. Baada ya hayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amezielezea hali za watu katika kupokea kwao uongofu wa Qurani. Kisha Akazitaja sifa za Waumini katika mahusiano yao na ubinadamu, na tabia za makafiri na ushupavu wao kushikilia kutaka miujiza isiyokuwa Qurani juu ya ubora wake wa cheo, na juu ya kejeli zao mbali kabisa dhidi ya Mtume wao. Na Akamweleza Mtume kuwa Mitume wa kabla yake pia walifanyiwa kejeli! Pia ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kusimamia vitu vyote na nafsi zote, na kwamba Yeye ndiye Mwenye kumlipa kila mtu kwa anavyostahiki, na kwamba Qurani ndio muujiza mkubwa kabisa utakaobaki mpaka siku ya kiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Anayewapa nguvu Mitume Wake kwa miujiza Aitakayo. Na ikiwa washirikina wanaukanya utume wa Nabii, basi Mwenyezi Mungu Anashuhudia ukweli wake, na Yeye ndiye Mwenye kutosheleza kwa hayo.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map