Qurani
/
9- SURAT AT TAWBAH/
Aya 3
3- Na tangazo hili linatoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa watu wote wanapojumuika siku ya hija kubwa ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajitenga na dhima katika mapatano na washirikina waliofanya hiana. Basi enyi washirikina mliovunja! Mkirudi mkaacha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi itakuwa kheri kwenu hapa duniani na kesho akhera. Lakini mkikengeuka na mkabakia hivyo hivyo mlivyo, basi jueni kwamba nyinyi mngali chini ya Utawala wa Mwenyezi Mungu. Ewe Mtume! Waonye makafiri wote kuwa ipo adhabu iumizayo sana.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map