Qurani
/
10- SURAT YUNUS/
Aya 39
39- Bali washirikina hawa, wamekimbilia kuikadhibisha Qurani bila ya kuzingatia, wakajua kwanza ni yapi yaliyomo ndani yake! Wao wenyewe hawakutizama ina nini wala hawakusita kuitafuta tafsiri yake na kutaka kuzielewa hukumu zake kwa kuwauliza wengine. Na kwa njia hii hii ya kukadhibisha bila ya ujuzi, ndivyo makafiri wa kaumu zilizotangulia walivyowakanusha Mitume wao na Vitabu vyao! Basi ewe mwanadamu! Angalia yaliishiaje mambo ya wakadhibishaji waliotangulia. Waliachiliwa mbali na wakateketezwa kwa adhabu! Na huu ndio Mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa mfano wa watu hao.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map