Main Page

Download
About Islam
Islamic Pillars
Prophetic Tradition
Islamic Encyclopedia
Non-Muslims
Legislation
Creed
Prophet's Stories
Islamic history
Islamic Architecture
Library
Islamic conferences
Islamic conferences
   Qurani /10- SURAT YUNUS/
 
Introduction

(Imeteremka Makka na aya zake 109)

Sura hii ni ya Makka na imeteremka Makka. Ina aya 109. Imeanza kwa 
kuashiria cheo cha Kitabu hiki Kitukufu na yale wayasemayo washirikina 
yaliyomhusu Nabii (S.A.W). Kisha ikataja ulimwengu na Ishara za 
Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizomo humo, na malipo ya siku ya kiyama, 
na Mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwatendea makafiri, 
na kuwakemea kwa itikadi zao hizo, na hali ya watu wakati wa shida na 
neema, na Uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na kutoweza 
masanamu kufanya lolote. Na ndani ya sura hii, kuna ishara ya 
kuwakomoa makafiri kuwataka walete sura moja walau ya kuzua. Na pia 
ndani yake, kuna vitisho vikali vya Adhabu ya Mwenyezi Mungu 
Mtukufu, na hali za nafsi za watu, na jinsi Mwenyezi Mungu 
Anavyovichunguza vitendo vyao.
Kisha baada ya hayo, sura ikaingia kumwondolea Nabii (S.A.W) 
kuungulika kwake kwa ukafiri wao, pamoja na kutoa hoja ya kuwavunja 
kabisa, na ikampoza kwa kumtajia visa vya Manabii wengine na kaumu 
zao. Kikaja kisa cha Nuhu, na kisa cha Musa, Haruni, Firauni na Wana 
wa Israili. Kisha kikaashiriwa kisa cha Yunus, na kwa jina hilo sura hii 
ikaitwa. Na mwisho kabisa, sura hii imeelekea kubainisha mambo ya 
Mtume huyu ili kutimiza mawaidha na mazingatio.

        Next


(Imeteremka Makka na aya zake 109) Sura hii ni ya Makka na imeteremka Makka. Ina aya 109. Imeanza kwa kuashiria cheo cha Kitabu hiki Kitukufu na yale wayasemayo washirikina yaliyomhusu Nabii (S.A.W). Kisha ikataja ulimwengu na Ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizomo humo, na malipo ya siku ya kiyama, na Mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwatendea makafiri, na kuwakemea kwa itikadi zao hizo, na hali ya watu wakati wa shida na neema, na Uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na kutoweza masanamu kufanya lolote. Na ndani ya sura hii, kuna ishara ya kuwakomoa makafiri kuwataka walete sura moja walau ya kuzua. Na pia ndani yake, kuna vitisho vikali vya Adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hali za nafsi za watu, na jinsi Mwenyezi Mungu Anavyovichunguza vitendo vyao. Kisha baada ya hayo, sura ikaingia kumwondolea Nabii (S.A.W) kuungulika kwake kwa ukafiri wao, pamoja na kutoa hoja ya kuwavunja kabisa, na ikampoza kwa kumtajia visa vya Manabii wengine na kaumu zao. Kikaja kisa cha Nuhu, na kisa cha Musa, Haruni, Firauni na Wana wa Israili. Kisha kikaashiriwa kisa cha Yunus, na kwa jina hilo sura hii ikaitwa. Na mwisho kabisa, sura hii imeelekea kubainisha mambo ya Mtume huyu ili kutimiza mawaidha na mazingatio.

 
Main Page Contact us Links About us Site Map