Qurani
/
12- SURAT YUSUF/
Aya 19
19- Wakaja watu upande ule wa kisima katika msafara wao wa kwendea haraka Misri. Wakamtuma mtu kati yao wa kuchota maji ya kunywa kisimani awaletee. Akatumbukiza ndoo yake akaivuta na mara ghafla akamwona Yusufu kanganganilia. Mchota maji yule akapiga kelele za furaha: Heri! Habari gani hii ya furaha! Huyu ni kijana! Wakamficha katika vitu vyao, wakamfanya ni bidhaa ya kuuzwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka yote waliyokuwa wakiyatenda kwa ujuzi Wake.
Main Page
Contact us
Links
About us
Site Map